Diamond Platnumz amemtaja Vanessa Mdee kama muimbaji anayemkubali zaidi na ambaye anaona atafika mbali zaidi.

Akiongea na Bongo5, Diamond amesema hata jukwaani, Vanessa ni msanii anayejituma sana.
“Unajua
wasanii wa kike wote wa hapa nyumbani ninawakubali ila namkubali sana
Vanessa. Na hata nikikutana naye huwa namwambia kuwa ‘Vanessa unanipa
imani sana kuwa tuna mwanamuziki wa kike ambaye naona kabisa anabadilika
kila siku na anajituma sana hata akiwa kwenye stage’. Unaona kabisa ana
juhudi zaidi maana Vanessa alikuwa akiimba kizungu sana lakini kila
siku zinavyoenda anabadilika na anaelewa nini anafanya sio mtu wa
kujitoa fahamu,” alisema.
“Kwahiyo
nina imani ipo siku tutaona msanii wa kike kutoka Tanzania anafanya
vizuri. Kwahiyo Vanessa namkubali sana na nina imani atafika mbali, ni
mfano mzuri sana pia na kwa wengine kujituma zaidi na kuwa wabunifu wa
kazi.
No comments:
Post a Comment