
Diamond Platnumz ametajwa kuwania tuzo nyingine za kimataifa
zinazofahamika kama ‘THE HEADIES 2014’, ambazo ni tuzo kubwa nchini
Nigeria.
Nasib Abdul ametajwa kuwania kipengele cha Msanii Bora wa Afrika (Best
African Arstist) ambacho kinawaniwa na wasanii wa nje ya Nigeria. Katika
kipengele hicho anashindana na Mafikizolo, Sarkodie na R2Bees.
Tuzo hizo zinatarajiwa kufanyika October 25, 2014.
Wasanii wengine wa Nigeria waliotajwa kuwania tuzo hizo katika vipengele tofauti ni pamoja na Davido, Wizkid, 2Face, Tiwa Savage, KCee, Burna Boy na wengine.
Ingia hapa kupata orodha kamil
No comments:
Post a Comment