Baada ya kuhusishwa na tetesi za kusaini na lebo ya Jay Z, Roc Nation muimbaji wa Nigeria, Tiwa Savage ameanza kuthibitisha kuwa ni mmoja kati ya watu wa familia hiyo.
Ni zaidi ya miezi miwili iliyopita muimbaji huyo alionekana akiwa nchini Marekani pamoja na bosi wake wa lebo ya Mavin Records, Don Jazzy walipotembelea ofisi za Roc Nation na kupiga picha na Jay Z lakini tangu hapo wamekuwa kimya kuzungumzia kinachoendelea.
Kupitia mtandao wa Instagram, Tiwa Savage ameweka picha akiwa na Dj Khaled ambaye pia ni msanii wa lebo hiyo na kuandika, “RocNation Family .”
Tiwa Savage na Don Jazzy walipotembelea ofisi za Roc Nation mwezi Juni mwaka huu
Balozi huyo wa Forte Oil, MTN na Pepsi atakuwa msanii wa kwanza kutoka Afrika kusainishwa kwenye label hiyo na kujiunga mastaa ambao wapo chini ya lebo hiyo akiwemo Dj Khaled, Rihanna, Big Sean na wengine.
No comments:
Post a Comment