Thursday 15 September 2016

Birdman adai Lil Wayne ameihodhi album ya ‘Tha Carter V’

Birdman amedai kuwa Lil Wayne, ameihodhi album yake ya ‘Tha Carter V.’
lil-wayne-birdman
Vyanzo vilivyo karibu na Birdman vimeiambia TMZ kuwa vitisho vya Wayne kuacha muziki vimemshtua bosi huyo wa Cash Money, anayedai kuwa madai kuwa ameishikilia album hiyo si ya kweli.
Vimesema ni Weezy ndiye mwenye kopi ya master ya album hiyo, na hivyo Birdman anaona kama hahusiki nayo tena. Kwa upande wa Wayne, imedaiwa kuwa yuko tayari kuwapa album hiyo lakini hadi alipwe chake.
Pia vyanzo hivyo vimedai kuwa Weezy hatoivujisha album hiyo kwasababu hana mpango wa kuitoa bure. Awali, Wayne alidai dola milioni 8 kama advance na pia ikikamilika angepewa dola milioni 2. Kama atapewa kiasi hicho cha fedha, basi album hiyo itatoka.
Wiki hii Lil Wayne alidai kuwa hawezi kuacha muziki lakini hatofanya tena kazi na Birdman.

No comments:

THIS BLOG DESIGNED BY

HOME BOYZ GRAPHICS LABORATORY