Thursday 1 September 2016

Chris Brown atoka jela kwa dhamana

Chris Brown yupo nje kwa dhamana.
Chris-Brown-2016-ppcorn
Chris-Brown-2016-ppcorn
Muimbaji huyo ametoka kwa dhamana ya $250,000 usiku wa Jumanne baada ya kukamatwa kwa madai ya kumtishia mtu na silaha.
Baylee Curran alimshutumu Brown kwa kumtishia na bunduki yake huko Tarzana, Calif. Mrembo huyo aliyekuwa akijirusha na Brown kabla ya hapo, anadai kuwa ugomvi ulizuka baada ya kuonesha kutamani midani zake za madini.
Muimbaji huyo alidaiwa kumfukuza msichana huyo na kumtishia na bunduki.
Maofisa wa polisi waliwasili kwenye eneo la tukio saa tisa alfajiri Jumanne hii baada ya simu ya 911 kupigwa na mwanamke aliyehitaji msaada. Curran alipeleka mashtaka polisi na kukatolewa hati ya kufanywa msako.
Wakati wa uchunguzi, Brown anadaiwa kutupa begi lake dogo nje ya dirisa ambamo kulikuwa na bunduki mbili na madawa, kwa mujibu wa mtandao wa TMZ.
Baada ya kulitupa, Breezy anadaiwa kupiga yowe ‘come and get me.’
Brown atapanda kizimbani Sept. 20 na bado anakana mashtaka hayo.

No comments:

THIS BLOG DESIGNED BY

HOME BOYZ GRAPHICS LABORATORY