Monday 3 October 2016

Soundtrack ya Karibu Kiumeni kuwakutanisha Nature na Inspekta kwa mara kwanza tangu ‘Mzee wa Busara’

Katika collabo zilizowahi kutikisa uga wa Bongo Flava, Mzee wa Busara ya Juma Nature na Inspekta Haroun haiwezi kukosa kwenye 50 bora za muda wote.
14063482_1087105781374957_1344463392_n
Ernest Napoleon akiwa kwenye set ya filamu hiyo na Idris Sultan
Ni kwasababu ilikutanisha mahasimu hao wa Temeke kwa mara ya kwanza tangu kuwepo kwa bifu lao lililochagizwa na harakati za kila mmoja kuutetea ufalme wa TMK. Nguvu yake enzi hizo, ilikuwa ni sawa kama leo Diamond na Alikiba wafanye ngoma ya pamoja.
Na sasa, tarajia kuwasikia wakali hao kwenye ngoma nyingine, wakionesha umwamba wa Rap Katuni, na tena mpishi akiwa yule yule, Mdachi anayewawezea, P-Funk. Hiyo ni kwa hisani ya filamu ijayo, Karibu Kiumeni, inayochezwa na Ernest Napoleon.
“Ngoma zitakuwa kama sita, moja itakuwa Nature na Inspekta, watafanya ngoma itakayobeba jina la movie na maudhui ya Temeke,” Napoleon ameiambia Bongo5.
“Itakuwa ngoma ya kwanza ya kurap pamoja tokea Mzee wa Busara,” ameongeza.
Napo amesema kwenye soundtrack hiyo, TID atafanya ngoma na Adili huku Fid Q akifanya na AY.
Ameendelea kufafanua, “Damian Soul pia atafanya Ngoma ya mapenzi, halafu Msaga Sumu Sengeli. Wengine watakuwepo kama Young Killer, Dogo Janja, watafanya ngoma ya pamoja ya generation yao.”
Filamu hiyo imewakutanisha pia Idris Sultan, Irene Paul, Muhogo Mchungu, Rashid Matumla na wengine. Chini ni baadhi ya picha za location.
14033618_645366765639458_234398868_n

14156568_737521563055307_1453604254_n
14280652_155551024889325_331026568_n


No comments:

THIS BLOG DESIGNED BY

HOME BOYZ GRAPHICS LABORATORY