Thursday 15 March 2018

Ahukumiwa jela kwa kumuua mpenzi wake kisa Youtube

Habari kutoka nchini Marekani ni kwamba binti mmoja amehukumiwa kifungo jela baada ya kumuua mpenzi wake wakati wakicheza mchezo wa kudanganya watu kwenye mtandao wa Youtube ili wapate followers wengi. Inaelezwa kuwa ‘prank’ hiyo ambayo ilikuwa imeandaliwa na wapenzi hao Monalisa Perez, 20, na Pedro Ruiz, 22, ililenga kufanya kama kijana huyo Pedro amepigwa risasi na Monalisa ili kwamba video hiyo isambae sana mtandaoni. Mpango huo haukufanikiwa kwani binti huyo alipofyatua risasi ambayo walipanga ipige kwenye kitabu kikubwa ambacho alikuwa amekishika kijana huyu, risasi hiyo ilipenya moja kwa moja na kwenda kumpiga kijana huyo kifuani na kufa papo hapo. Binti huyo ambaye ni mama wa watoto wawili amehukumiwa kifungo cha miezi sita kwa kuua bila kukusudia.

No comments:

THIS BLOG DESIGNED BY

HOME BOYZ GRAPHICS LABORATORY