Huu ni wimbo mpya kabisa, umepewa jina la “Mahaba Niue” ikiwa ndio ‘singo’ mpya ya albam ijayo ya Jahazi Modern Taarab.
Ni utunzi na uimbaji wake Mfalme Mzee Yussuf, ngoma kali ambayo inakuwa zawadi nzuri ya kufungia mwaka 2014 na kufungua 2015.
Kazi
hii imefanyika katika studio za Sound Crafters, Temeke jijini Dar es
Salaam, chini ya producer Enrico. Ndani ya wimbo huu utakutana na mipini
mikali ya Mohamed Mauji aliyetambaa vizuri na gitaa lake la solo huku
kwenye kinanda kazi kubwa ikiwa imefanywa na Chid Boy.
Kama
ilivyo kawaida ya Mzee Yussuf kwenye ngoma chini ambapo hufunika na
vionjo vikali, humu nako ametisha sana, utakutana na vitu vya “Songa
Ugali Tule” na vikorombwezo vingine kibao.
Je huu ndio wimbo wa mwisho wa Mzee Yussuf? Sahau kabisa hiyo kitu. Mzee Yussuf ameiambia Saluti5 kuwa lolote linaweza kutokea.
“Ningependa
kuacha kuimba mwaka huu, lakini ni mapokeo ya kazi hii ndiyo
yatakayoamua, nitaangalia mashabiki wanaipokea vipi, nitaangalia pia
namna malengo yangu mengine yatakavyokuwa.
Ninatamani
“Mahaba Niue” uwe wimbo wangu wa mwisho, lakini sisemi kuwa huu ni
wimbo wangu wa mwisho,” alisema Mzee Yussuf katika maongezi yake na
Saluti5.
No comments:
Post a Comment