Katika
ripoti iliyotoka jana kuhusu utafiti uliofanywa na Economists
Intelligence Unit ya nchini Uingereza, ndugu Edward Lowassa kaongoza
tena katika utafiti huo. Sehemu ya ripoti hiyo inaeleza ya kwamba
Lowassa ndiye mwanasiasa anayekubalika zaidi ndani ya chama cha
Mapinduzi (CCM) kwa kuwania urais 2015.
Economist
Intelligence Unit ni moja ya taasisi/kitengo bora duniani katika
maswala ya kiitafiti kwenye nyanja mbali mbali likiwemo maswala ya
uchaguzi.
Tarehe
26/11/2007, kitengo hiki kilitoa ripoti ya utafiti wao kuhusu uchaguzi
wa Marekani ya kwamba Obama ataibuka mshindi katika uchaguzi wa 2008.
Matokeo nafkiri tunayajua....
Tarehe
14/10/2012, kitengo hiki hiki kilitoa ripoti kuhusu uchaguzi wa nchini
Ghana, ya kwamba John Mahama ataongoza katika uchaguzi huo na ndiye
alikuwa chaguo la wananchi. Matokeo wote tunayo....
Tarehe
24/10/2014, kitengo hiki hiki kilitoa ripoti kuhusu uchaguzi wa nchini
Brazil. Katika ripoti hiyo mgombea Dilma Rouseff aliibuka mshindi kama
kitengo hicho kilivyotoa ripoti yake ya kiutafiti..
Jana
tarehe 20/12/2014, kitengo hicho kimetoa ripoti ya utafiti kuhusu
uchaguzi wa mwakani hapa nchini. Na kumpa Lowassa ushindi mkubwa sana...
Mytake:
chonde chonde tusithubutu hata kidogo kutupilia mbali maoni ya
wananchi. Uchaguzi wa 2002 nchini Kenya, chama cha KANU kilipuuza maoni
ya wananchi na hatimaye matokeo leo hii tunayo vichwani mwetu. Sauti ya
wananchi ni kubwa sana ingawa unaweza usiione mpaka pale utakapo pata
pigo takatifu.
Huu
ni utafiti wa tatu mfululizo unaowagusa wananchi. Ni wito kwa CCM
kusoma alama za nyakati na kusikia sauti za wananchi. Kura za maoni ni
sauti za wananchi.
Source: magazeti ya leo (Mtanzania)..
Asante
Ocampo four

No comments:
Post a Comment