Wednesday 8 June 2016

Bifu ya Prezzo na Jaguar


Prezzo amchana Jaguar, amuita mshamba, ni baada ya yeye kuitwa ‘socialite’ (Audio)


Wiki kadhaa zilizopita, Jaguar alihojiwa kwenye kituo cha redio cha Kenya, Kiss FM na kudai kuwa Prezzo ni socialite wa kiume anayependa sifa.

 Tafsiri ya socialite ni: Someone who has money and doesn’t work, instead devoting his/her life to being “socially active.” Socialites go to parties, gather media attention, and essentially “work” at being popular.

“Mimi simchukii Prezzo namheshimu sana lakini akicome tufanye song aache hiyo mambo ya usocialite ana akue mwanaume,” alisema Jaguar kwenye interview hiyo.

Kwa upande wake Prezzo aliyezungumza hivi karibuni na kipindi cha Funiko Base cha Radio5, alidai kuwa hana tatizo na wazo hilo la kufanya wimbo naye lakini akamuonya apunguze kwanza ushamba.
“Akipunguza ushamba then mimi na yeye tunaweza kufanya kazi. Lakini ujue jamaa kwangu mimi ana ushamba mwingi yaani. Kuna video kafanya na Mafikizolo angalieni hiyo nyimbo. Kuna sehemu kafanya kile kitu kinachofaa kuwa dub. Ile Jaguar alivyofanya mshkaji wangu ni kama anampiga mtu kipepsi,” alisema Prezzo na kumalizia na kicheko.

No comments:

THIS BLOG DESIGNED BY

HOME BOYZ GRAPHICS LABORATORY