Wednesday 7 March 2018

VIDEO | Chief Maker - Sogea | Download Mp4 [Official Video]

https://cldup.com/CzlFCZP0lr.mp4?download=Chief%20Maker%20-%20Sogea%20@%20BOYCHEEDY.COM.mp4
Read more »

Audio | Nash MC - Maneno | Download Mp3 [New Song]

Read more »

INSTRUMENTAL | Mbosso - Shida (BEAT) | Download Mp3

Shida (BEAT) Mbosso - Shida (BEAT) INSTRUMENTAL | Mbosso - Shida (BEAT) | Download Mp3
Read more »

Friday 2 February 2018

Trump awapatia maelfu ya wakimbizi kutoka Syria ruhusa kuishi Marekani

Serikali ya Rais Donald Trump imeongeza kinga ya muda kwa karibu wakimbizi 7,000 wa Syria wanaoishi nchini Marekani wakati vita vikiendelea nchini mwao.
Walikuwa wamepewa kinga ya muda dhidi ya ya kurejeshwa nyumbani chini ya mpango wa kibinadamu unaofahamika kama -Temporary Protected Status (TPS).
Rais Trump amefuta mpango huo kwa nchi mbali mbali katika kipindi cha miezi ya hivi karibuni, na hivyo kuwaathiri wahamiaji kutoka kutoka El Salvador, Haiti na Nicaragua.
Image caption Waziri wa usalama wa ndani wa Marekani Kirstjen M Nielsen anasema kuwa Marekani itachunguza maombi ya kila nchi kwa kuzingatia hali ya nchi husika
Marekani ilisema kuwa haitakubali maombi ya wahamiaji kupitia TPS kutoka Syria.
"Ni wazi kwamba hali iliyoyopelekea Syria kuchaguliwa ina msingi wa kuendelea kuwepo, kwa hivyo kurefushwa kwa muda wa kinga kwa wakimbizi kunakubalika chini ya sheri ," alisema waziri usalama wa ndani Kirstjen M Nielsen katika taarifa yake.
"Tutaendelea kuchunguza maombi ya kila nchi kwa kuzingatia hali ya nchi husika. Kwa raia wa Syria ambao tayari wanaishi na kufanyia kazi nchini Marekani, mpango wa TPS utarefushwa kwa miezi mingine 18. Lakini Wasyria walioingia nchini Marekani baada ya Agosti 2016 watatengwa na mpango huo licha ya kuendelea kwa hali mbaya nyumbani."
Mpango wa hadhi ya ulinzi kwa raia wa Syria ulipangwa kufikia kikomo tarehe 31 Machi.
Mapema mwaka huu, Wizara ya Usalama wa Ndani ilitangaza kuwa itafikisha kikomo mpango wa kinga kwa raia 262,500 kutoka El Salvador, ingawa hatua hiyo itacheleweshwa kwa miezi 18.
Mwezi Novemba, utawala huo ulisema kuwa hadhi ya ukimbizi ya raia takriban 59,000 wa Haiti itakwisha 2019
Read more »

Mwanamuziki wa Uganda Mowzey Radio afariki dunia

Mwanamuziki wa Uganda Moses Ssekibogo, anayefahamika zaidi kwa jina la Mowzey Radio wa kundi la Goodlyfe amefariki.
Bw Balaam Barugahara, ambaye ni promota, anasema kuwa Radio alifariki dunia Alhamisi majira ya saa kumi na mbili asubuhi.
Radio alifariki katika hospitali ya Case mjini Kampala ambako alikuwa amelazwa baada ya kuripotiwa kupigwa hadi kupoteza fahamu kwenye kilabu cha pombe cha De Bar, kilichopo katika mji wa Entebbe wiki iliyopita.
"Utawala wa hospitali ya Case wanasikitika kutangaza kifo cha Moses Ssekibogo alias Moze Radio leo tarehe 1 Februari 2018 saa kumi na mbili asubuhi," ilisoma sehemu ya taarifa iliyotolewa na Hospitali ya Case kuhusiana na kifo hicho.
"Nimeelezwa juu ya kifo cha mwanamuziki Moses Ssekibogo aka Mowzey Radio. Hivi karibuni nilitoa mchango wangu kwa ajili ya matibabu yake nikitumaini kwamba atapona. Alikuwa kijana mdogo mwenye kipaji mwenye maisha mazuri ya mbeleni," Alielezea Museveni katika ujumbe wa Twitter
Haki miliki ya picha Radio & Weasel
Image caption Mowzey Radio alikuwa anaimba pamoja na Weasel kama Radio & Weasel
Hii inakuja saa chache baada ya rais Museveni kuchangia Shilingi milioni 30m, pesa za Uganda kwa ajili ya matibabu yake.
''Wakati Mowzey Radio alipoingia kwenye uwanja wa Muziki, sekta ya muziki ilikua mahututi. Muziki wa wanamuziki wachache wa waliokuwa maarufu zaidi wakati huo ulikua umerudiwa rudiwa kupita kiasi na kuchosha .Ninyi wawili mlikuja kwenye sekta hii na kuiongezea uhai sekta ya muziki. Mlileta ushindanikwa miziki mizuri na uvaaji mpya ," Alituma ujumbe Liz Elder kwenye ukurasa wa Facebook.
Vipaji vya Radio vya Uimbaji pamoja na muziki vilianza kubainika wakati alipokuwa mwanafunzi katika shule ya sekondari, akiimba katika kwaya ya kanisa katoliki. Akiwa mwanafunzi wa sekondari pia aliweza kujizolea tunu mbali mbali za uimbaji katika ngazi ya wilaya na nyingine nyingi.
Radio alipendwa sana kwa utumbuizaji wake kwenye sherehe na tamasha mbali mbali za muziki na za kijamii kwa sauti yake thabiti na ya kuvutia.
Wiki iliyopita, polisi walisema kuwa waliwakamata watu watano kwa ajili ya kuisaidia katika uchunguzi wa polisi juu ya kisa cha kumpiga Radio.
Read more »

Kiongozi aliyekamatwa kwa kuhusishwa na kiapo cha Raila aachiliwa

Mbunge wa eneo bunge la Ruaraka nchini Kenya aliyehusishwa na kiapo cha kiongozi wa upinzani nchini humo Raila Odinga amewachiliwa kwa dhamana ya ksh.50,000 baada ya kulala katika seli za kituo cha polisi.
Tom Kajwang alifikishwa katika mahakama ya Milimani jijini Nairobi Alhamisi jioni ambapo alitarajiwa kukabiliwa na mashtaka yanayohusiana na kushiriki katika mkutano na kula kiapo kinyume na sheria.
Wabunge wa Nasa waliojaa katika mahakama hiyo walisema kuwa mashtaka aliyowekewa Kajwang ni bandia.
Kajwang alilala katika kituo cha polisi cha Kiambu baada ya kukamatwa siku ya Jumatano kwa kile maafisa wanasema ni jukumu lake katika sherehe ya kuapishwa kwa Raila Odinga kuwa 'rais wa wananchi'.
Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kiongozi aliyekamatwa kwa kuhusishwa na kiapo cha Raila aachiliwa
Mbunge huyo ambaye alisimama nyuma ya Raila wakati wa hafla hiyo iliofanyika katika uwanja wa Uhuru Park Jijini Nairobi alikamatwa katika mahakama ya Milimani jijini Nairobi na kupelekwa makao makuu ya ujasusi ili kuhojiwa.
Kesi yake itaendelea tarehe 6 wiki Ijayo.
Read more »

Magufuli ateua Mwanasheria mkuu mpya wa serikali

Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli amemteua Dokta Adelardus Kilangi kuwa Mwanasheria mkuu wa serikali.
Uteuzi huo umeanza jana, Februari mosi.
Kabla ya uteuzi huo Dokta Kilangi, alikuwa Mkurugenzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino, kituo cha Arusha, na pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Shughili za mkondo wa juu ya mafuta-PURA.
Wakati huohuo, Rais Magufuli amemteua Paul Ngwembe kuwa Naibu Mwanasheria mkuu wa serikali.
Kabla ya uteuzi huo alikuwa Paul Ngwembe, Mkurugenzi wa masuala ya sheria katika Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania.
Kufuatia uteuzi huo, Rais Magufuli amewateua aliyekuwa Mwanasheria mkuu wa serikali George Mcheche Masaju na Aliyekuwa Naibu Mwanasheria mkuu wa serikali Gerson Mdemu kuwa Majaji wa Mahakama kuu.
Uteuzi huo pia umeanza jana Februari mosi
Read more »

Marekani yamshutumu Odinga kwa 'kujiapisha' Kenya



Serikali ya Marekani imesema imesikitishwa na hatua ya kiongozi wa upinznai nchini Kenya Raila Odinga ya kujiapisha Jumanne wiki hii.
Marekani pia imeishutumu serikali kwa kufungia vituo vinne vya habari nchini humo ambavyo viliadhibiwa baada ya kupeperusha moja kwa moja hafla hiyo ya upinzani.
Kupitia taarifa, wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema taifa hilo linaamini mizozo yoyote ile inafaa kutatuliwa kwa njia zifaazo kisheria.
"Tunakataa vitendo vyovyote ambavyo vinahujumu Katiba ya Kenya na utawala wa sheria. Uhuru Kenya alichaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Kenya mnamo Oktoba 26, 2017 katika uchaguzi ambao uliidhinishwa na Mahakama ya Juu," taarifa hiyo iliyotumwa na msemaji wa wizara hiyo Hearther Nauerth imesema.
Bw Odinga alisusia uchaguzi huo wa marudio na amesema hamtambui Rais Kenyatta kama rais halali wa taifa hilo.
Jumanne, alikula kiapo kuwa Rais wa Wananchi katika hafla iliyohudhuriwa na maelfu ya wafuasi wake uwanja wa Uhuru Park, Nairobi.
Mgombea mwenza wake Kalonzo Musyoka, ambaye ni makamu wa rais wa zamani, hakuhudhuria sherehe hiyo ingawa walikuwa wameahidi kuapishwa wote wawili kwa pamoja.
Image caption Wafuasi wa Bw Odinga wakisherehekea Kisumu baada yake kula kiapo Uhuru Park, Nairobi
Bw Musyoka baadaye alisema alipokonywa walinzi wake na hivyo kuzuiwa kuondoka nyumbani kwake kwenda kuhudhuria sherehe hiyo.
Bw Odinga alipokuwa anakula kiapo alisema Bw Musyoka angeapishwa baadaye.
Jumatano, mbunge wa upinzani Tom Joseph Kajwang' anayewakilisha eneo bunge la Ruaraka, Nairobi alikamatwa na akashtakiwa kwa makosa ya kuhudhuria mkutano haramu na kushiriki katika kulishwa kiapo kwa Bw Odinga kwa njia ya kudai kumfunga Bw Odinga "kutekeleza kosa la jinai la uhaini".
Bw Kajwang', ambaye ni wakili, alikuwa amevalia sare za uwakili na kwa pamoja na mshauri wa zamani wa Bw Odinga, Miguna Miguna, walikuwa karibu na Bw Odinga alipokuwa anakula kiapo.

Kufungiwa kwa vituo vya habari

Marekani imesema imesikitishwa sana na vitendo vya serikali kwa "kufunga, kutisha na kuminya vyombo vya habari".
"Uhuru wa kujieleza, ikiwa ni pamoja na kwa wanahabari, ni muhimu sana kwa demokrasia, na umelindwa kwenye Katiba ya Kenya," taarifa ya Marekani imesema.
"Tunaihimiza serikali na Wakenya wote kuheshimu uhuru wa kujieleza na kutii agizo la mahakama na kuvifungulia vituo hivyo vya televisheni."
Mahakama ilikuwa imeamuru vituo hivyo vya Citizen, Inooro, NTV na KTN vifunguliwe Alhamisi lakini kufikia Ijumaa asubuhi, agizo hilo lilikuwa bado halijatekelezwa.
Ingawa Marekani imewasifu polisi na vikosi vya usalama kwa jinsi walivyosimamia hafla hiyo ya kuapishwa kwa Bw Odinga Jumanne, wamesema visa vya kukamatwa na kushtakiwa kwa washukiwa vinafaa kutekelezwa kwa kufuata sheria kikamilifu.
Marekani imewahimiza viongozi wa kisiasa Kenya kufanya mazungumzo kwa lengo la kuimarisha uwiano na utangamano na kutatua matatizo ya muda mrefu nchini humo.
Read more »

Wachimba mgodi 955 waliokwama Afrika Kusini waokolewa

  • 2 Februari 2018
Haki miliki ya picha AFP / Getty Images
Image caption Mchimba mgodi aliyeokolewa akiondolewa eneo hilo kwa basi
Wachimba mgodi wote 955 waliokuwa wamekwama katika mgodi mmoja wa dhahabu ulioko mkoa wa Free State nchini Afrika Kusini wameokolewa wakiwa salama.
Walikuwa wamekwama ndani ya mgodi huo baada ya umeme kukatika Jumatano usiku.
"Kila mtu ametolewa," James Wellsted, msemaji wa kampuni inayosimamia shughuli kwenye mgodi huo ya Sibanye-Stillwater amesema.
Ameeleza kuwa kuna visa kadha vya "watu kupungukiwa na maji mwilini na shinikizo la damu, lakini hakuna aliye na tatizo kubwa."
Mgodi huo wa dhahabu wa Beatrix unapatikana kilomita 300 Kusini Magharibi mwa Johannesburg na una ngazi 23 ambapo hufika hadi mita 1,000 chini ya ardhi.
Chanzo cha wachimba migodi hao kukwama ilitokana na mvua kubwa iliyonyesha nyakati za usiku wakati wachimba migodi hao walipokua chini ya mgodi huo na kuangusha nguzo ya umme iliyosababisha umeme kukatika
Afrika Kusini inaongoza kwa uchimbaji wa madini lakini usalama katika migodi umekuwa wa kutiliwa shaka.
Lakini Ijumaa subuhi, umeme ulirejeshwa na kuwezesha wafanyakazi hao kuokolewa.
"Ilikuwa hali ya kutisha, hakukuwa na hewa ya kutosha," mmoja wa wachimbaji mgodi hao Mike Khonto amesema.
"Twashukuru wasimamizi kwamba waliweza kututumia chakula na maji."
Wafanyakazi hao wamepelekwa kula chakula na kuoga kabla ya kufanyiwa uchunguzi wa kiafya na kisha kuruhusiwa kuondoka.
Image caption Umeme umerejeshwa eneo hilo
Jamaa za wachimba mgodi hao walikuwa wamekusanyika barabara ya kuelekea kwenye mgodi huo lakini wakadhibitiwa na vikosi vya usalama.
Maafisa wa vyama vya wachimba mgodi awali walikuwa wamelalamika kwamba maisha ya wafanyakazi hao yalikuwa hatarini.
Watu zaidi ya 80 walifariki kwenye migodi Afrika Kusini mwaka 2017.
Read more »

Mzee Kingunge Ngombale Mwiru amefariki dunia alfajiri ya leo




Taarifa zilizotufikia hapa Ayo TV na millardayo.com asubuhi hii ya leo ya February 2, 2018 ni kwamba Mwanasiasa mkongwe Mzee Kingunge Ngombale Mwiru amefariki dunia alfajiri ya leo.
Mzee Kingunge alikuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kushambuliwa na mbwa nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam takriban mwezi mmoja uliopita.
Mke wa Kingunge Peras Ngombalemwiru alifariki dunia mwanzoni mwa mwezi January kutokana na ugonjwa wa kupooza kipindi ambacho Mzee Kingunge alikuwa tayari anapatiwa matibabu ya majeraha hayo.
Katikati ya mwezi January mtoto wa marehemu, Kinjekitile aliiambia Ayo TV kuwa hali ya baba yake ilikuwa ikiendelea kuimarika kasoro miguu ambayo bado ilikuwa ikisumbua.
Muhimbili Hospitali wazungumzia Hali ya Mzee Kingunge
Read more »

Mtoto wa kwanza wa Fidel Castro amejiua



Taarifa iliyoshika headlines kwenye vyomba vya habari nchini Cuba ni kuhusu Mtoto wa Mwanamapinduzi na aliyekuwa Rais wa Cuba Fidel Castro, Fidel Ángel Castro Díaz-Balart, mwenye umri wa miaka 68 amejiua akiwa mji mkuu wa Havana.
Amekutwa amefariki February 1, 2018 na inadaiwa alikuwa anatatizwa na msongo wa mawazo. Castro Díaz-Balart alifahamika sana kama “Fidelito” na alikuwa mtoto wa kwanza wa rais huyo wa zamani wa Cuba aliyefariki dunia November 2016.

Alikuwa mshauri wa kisayansi wa Baraza la Serikali ya Cuba na alihudumu kama makamu rais wa Chuo cha Sayansi cha Cuba pia alifanya kazi kama Mwanafizikia ya nyuklia.
Gazeti rasmi la Serikali ya Cuba la Granma limeandika hivi>>> “Fidel Castro Diaz-Balart, aliyekuwa ametibiwa na kundi la madaktari kwa miezi kadha kutokana na msongo wa mawazo, alijitoa uhai asubuhi hii,”
Runinga ya taifa imesema amekuwa akipokea matibabu miezi ya karibuni kama mgonjwa wa kutibiwa na kurudi nyumbani, baada yake kulazwa hospitalini kwa muda.
Read more »

Thursday 4 January 2018

Waziri Njemba atoa agizo hili kwa wasiokuwa na kitambulisho cha Taifa

Waziri Njemba atoa agizo hili kwa wasiokuwa na kitambulisho cha Taifa

 13:46 

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dr. Mwigulu Nchemba akiwa kwenye ziara ya kikazi mkoani Ruvuma ameagiza kila mtanzania kujiandikisha kupata kitambulisho cha taifa kwakuwa sio jambo la hiari bali ni lazima kwa kila Mtanzania aliyeko ndani ya mipaka ya nchi kutambuliwa.

“Hili zoezi la vitambulisho vya utaifa ni lalazima kwa kila mtanzania aliye nchini, ni kosa kubwa kama wewe ni raia ukaamua kukaidi ikiwa Rais wetu Magufuli ameamua kutoa vitambulisho hivyo bure bila malipo yoyote”–Dr Nchemba

“Hili ni jambo la Nchi na ni kubwa hivyo tusililinganishe na jambo lingine lolote, baada ya mchakato huu kuisha tukamkuta mtu hana kitambulisho maelezo yake yatakuwa ni magumu kueleweka kama kweli yeye ni mtanzania halali” –Dr Nchemba
Read more »

Uchangudoa wa Zari Waibua Kimbembe

Uchangudoa wa Zari Waibua Kimbembe

 10:00  
MAMBO ni moto! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya mfanyabiashara maarufu Afrika Mashariki, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kukiri kuwa yeye ni changudoa mzee, kauli yake imeibua kimbembe.

KUPITIA SNAPCHAT
Kupitia mtandao wake wa kijamii wa Snapchat, mwishoni mwa wiki iliyopita, Zari alitupia ujumbe akionesha kuwa yeye ni changudoa mzee, lakini mwenye mafanikio akimjibu hasimu wake, mwanamitindo Hamisa Mobeto bila kumtaja. “Bora mimi changudoa mzee niliye na mafanikio na bado ananipenda kuliko kijana wa miaka 20+, mama uliyeachwa mara mbili na tuzo juu,” alisema Zari kupitia Snapchat. Kwa muda mrefu, Zari amekuwa kwenye tifu la aina yake baada ya Mobeto kuzaa na bwana wake, msanii wa Bongo Fleva miezi michache iliyopita.

KIBEMBE KILIVYOIBUKA
Kitendo cha Zari kutoa kauli hiyo, kimbembe kiliibuka mtandaoni mara baada ya ukurasa wa Instagram wa Global Publisher, kutupia habari hiyo ambapo wafausi wa mtandao huo walianza kurushiana maneno makali huku kila mmoja akitoa msimamo wake.

AUNGWA MKONO, AKOSOLEWA
Kuna ambao waliunga mkono kauli hiyo kwa kile walichosema kwamba aliandika kwa maana ya kumkejeli Mobeto, lakini si kwamba ni kweli yeye ni changudoa, lakini wengine walicharuka na kusema kweli yeye ni changudoa. “Jamani Zari siyo changudoa acheni kumshambulia kwa matusi. Yule amesema vile kama kumkejeli Mobeto ambaye aliingia kwenye anga zake, watu wengine sijui mkoje, mmekalia ujingaujinga tu,” alichangia shabiki mmoja mtandaoni akimkingia kifua Zari.
Baada ya shabiki huyo kumtetea Zari, wengine waliibuka na kumshambulia mama huyo wa watoto watano kwa kile walichosema kwamba kweli mrembo huyo wa Uganda ni changudoa aliyejivisha ‘ngozi’ ya ustarabu. “Acheni mambo ya kipuuzi…hivi mnafikiri Zari ana hela kama inavyodaiwa? Yule ni changuduoa tu kama walivyo machangu wengine na kama yeye mwenyewe alivyosema. Sema kinachompa hadhi yeye anajiuza kwa staha tofauti na wenzake wanaojipanga barabarani.

UTAJIRI WAKE WAHUSISHWA
“Kule Sauz (Afrika Kusini) mnavyoona anaishi kwenye majumba ya kifahari, anavyoonekana ana magari mapya kila siku mnafikiri yale ni jasho lake? Uchangudoa tu ule ndiyo unaompa utajiri wote alionao, yule msanii anajiona amepata kumbe amepatikana,” alisema shabiki huyo.
Mvutano huo ambao hadi tunakwenda mitamboni ulikuwa ukiendelea kwenye ukurasa huo wa Global Publishers unaaongoza kwa kutembelewa na watu wengi ndani na nje ya Bongo, ulisababisha watu kurushiana matusi ya nguoni huku wengine wakienda mbali kwa kutaka kutafutana uso kwa uso, nje ya mtandao huo wa Instagram ili wapeane ngumi kavukavu.

MWENYEWE AANIKA UKWELI
Baada ya kauli hiyo kuibua kimbembe, Zari amekuwa amewatolea uvivu kwa kuonesha namna ambavyo ni mchapakazi kupitia ofisi zake mbalimbali zinazomuingizia kipato halali tofauti na watu wanavyofikiri na kuweka mawazo yao kwenye mitandao ya kijamii.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Zari amekuwa akionesha picha za maduka yake ya nguo yaliyopo Afrika Kusini kwa kusindikiza na meseji mbalimbali zinazoashiria kwamba yeye si mtu wa mchezomchezo linapokuja suala la uwajibikaji. Ameonesha kwamba anatenga muda wake kwa kuwa bize na kazi, lakini pia anatenga muda wake kwa ajili ya kufurahia maisha kwa maana ya kuponda starehe katika viunga mbalimbali pande za Sauz na nyumbani kwao, Uganda.

ANA VYUO SAUZ
Kama hiyo haitoshi, kupitia mahojiano yake ambayo yapo kwenye mtandao wa Kijamii wa You Tube, Zari alifunguka kuwa anavyo vyuo vya urembo na masuala ya ulinzi. Pamoja na hayo, amekuwa amekuwa akizungumzia mafanikio mbalimbali anayoyapata kupitia matamasha yake makubwa hususan lile la Zari All White Party ambalo linampa mkwanja mrefu kila mwaka.
STORI: Erick Evarist, Dar IJUMAA WIKIENDA 
Read more »

Wasifu wa Mchora Katuni Masoud Kipanya

Wasifu wa Mchora Katuni Masoud Kipanya

Wengi humfahamu kwa jina la Masoud Kipanya, lakini hilo si jina lake halisi, tunaweza kusema hilo ni jina lake la sanaa kwani limetokana na na katuni za Kipanya ambazo huwa anachora.

Jina lake ni i Ali Masoud, jina la Kipanya ni matokeo ya katuni ya Kipanya aliyoibuni zaidi ya miaka 28 iliyopita. Alizaliwa tareha 23 Juni 1972 jijini Dar es salaam.

Kipanya alianza kuchora katuni akiwa darasa la pili, na alianza kwa kuiga tu katuni za ndani na za nje kama ilivyo kawaida kwa yoyote anayeanza kufanya kitu, ila ‘professionally’ alianza rasmi mwaka 1988, huo ndio mwaka ambao katuni yake ya kwanza ilitoka katika gazeti la Heko.

Amewahi kufanya kazi kama mhariri wa katuni kwenye gazeti la Sanifu na mhariri mtendaji wa katuni gazeti la majira, pia katuni zake hutokea gazeti la Mwananchi.

Licha ya kujizolea umaarufu mkubwa katika uchoraji katuni, katika familia yake hakukuwa na mchoraji kabla yangu, isipokuwa baada ya yeye, mdogo wake naye ameshaanza kuja juu katika fani ya katuni. Licha ya kuwa wazazi wake si wachoraji, lakini mfumo wa maisha yao unatosha kabisa kusema nao pia ni wasanii.

Akizungumzia kazi yake ya uchoraji katuni, Kipanya alisema kuwa, changamoto kubwa anayokumbana nayo ni censorship. Kwa wasioelewa, censorship ni ile kitendo ambacho unachora katuni halafu kabla haijachapishwa inapitiwa na kama itaonekana ina madhara kwa mtu ama jamii Fulani, basi itarekebishwa ama isichapishwe kabisa.

Amesema hayo yamemtokea mara nyingi tu katika maisha yake akiwa katika magazeti mbalimbali. Mara nyingi censorship hutokea pale inapoonekana unachora katuni zinazosumbua mioyo ya walengwa hususani wanasiasa wasiopenda kukosolewa.

Alipoulizwa kama amewahi kupata misukosuko kutokana na katuni zake, Masoud alisema, “nakumbuka siku niliyomchora mtu mnene akiwa amemshika kamba iliyomfunga mbwa ambaye ameandikwa ‘polisi’, maana ya katuni hii ukiangalia kwa haraka haraka ni kwamba jeshi la polisi haliko kwa manufaa ya umma bali kwa manufaa ya watu wachache hasa viongozi wa chama tawala.Hiki kilikuwa ni kile kipindi ambacho wapinzani walikuwa wakibughudhiwa na polisi kila walipotaka kufanya mikutano yao ya hadhara.”

“La pili ni wakati ule mbunge mmoja aliyejulikana kwa jina la Tuntemeke Sanga alipokuwa anaumwa, nilichora katuni inayomuonyesha mheshimiwa Sanga akiwa amelazwa huku akiwa ametundikiwa damu, halafu pembeni yuko serikali akiwa amegeukia upande mwingine huku akivuta sigara kana kwamba hajali, bahati mbaya siku iliyofuata Mzee Sanga akafariki, naikumbuka siku hiyo vizuri, aliyekuwa katibu wa bunge wa wakati huo, Mzee Mlawa, alivamia ofisi za gazeti la majira, bahati nzuri, wakati anaingia mimi nikawa natoka, na pengine kutokana na umbo langu, hakuweza kudhani kwamba pengine huyu ndio masoud kipanya. Kilichoendelea kati yake na mhariri wangu kwa kweli sikukifahamu.”

“Alarm inaniamsha saa 11 alfajiri, naoga, navaa na kuelekea studio. Naanza kipindi saa 12 mpaka 3 asubuhi, baada ya hapo napumzisha akili kwa kama nusu saa kwa kupitia magazeti mbalimbali then naanza kufikiria wazo la katuni, wakati mwingine kama sina wazo hunichukua mpaka nusu saa kudevelop wazo la katuni, by saa 4 asubuhi naanza kuchora editorial cartoon. Huwa natumia mpaka masaa mawili kutegemeana na aina ya katuni, baada ya hapo, saa sita mchana namkabidhi dereva (wa taxi, sio wangu jamani) apaleke katuni ofisi za gazeti la mwananchi kwa ajili ya kesho yake. Baada ya hapo nageukia upande wa illustrations, mara nyingi huwa nina kazi za taasisi mbalimbali za ku-Simplify text into cartoons kwa ajili popular versions za machapisho mbalimbali ya ndani na nje ya nchi. By saa 8 mchana huwa nimemaliza, kama kunakuwa na mikutano ofisini naingia, kwa kifupi by saa 10 jioni nakuwa nimemaliza ingawa wakati mwingine humaliza jioni zaidi, baada ya hapo narudi nyumbani kwa ajili ya kubadilisha nguo then naenda mazoezini. Nikitoka mazoezini huwa sitoki tena nyumbani,” alisimulia Kipanya wakati akijibu kuhusu ratiba yake kwa siku.

Kipanya, ameshiriki maonyesho mbalimbali Tanzania na Afrika Kusini kama mtaalam wa matumizi ya rangi ‘Painter’ na amejishindia tuzo nyingi ikiwa pamoja na tuzo ya kwanza ya katuni Afrika Mashariki.

Mbali na kuchora katuni, Kipanya ni mtangazaji wa kipindi cha Power Breakfast cha Clouds FM, ni mwanamitindo lakini pia ndiye mbunifu wa vipindi vya runinga vya ‘Maisha Plus’ na ‘Inawezekana.’ 
Read more »

Ikulu Yafunguka Kutoapishwa Kwa Dr Willibrod Slaa Baada ya Kuteuliwa Kuwa Balozi

Ikulu Yafunguka Kutoapishwa Kwa Dr Willibrod Slaa Baada ya Kuteuliwa Kuwa Balozi

WAKATI zikiwa zimetimia siku 40 baada ya kuteuliwa kuwa balozi, Dk. Willibrod Slaa (pichani), hajaapishwa na kuzua minong’ono hatimaye Ikulu imefunguka na kuweka kila kitu wazi.
Itakumbukwa kuwa Rais Dk. John Magufuli alitangaza uteuzi wa Dk. Slaa kushika nafasi ya ubalozi Novemba 23, mwaka jana, lakini tangu wakati huo hajaapishwa.

Rais Magufuli amekuwa na utamaduni wa kuteua viongozi na baada ya siku chache wanaapishwa, lakini kwa Dk. Slaa imechukua muda mrefu na kuibua sintofahamu.
“Hili ni jambo ambalo siyo la kawaida, tumezoea mtu akiteuliwa kushika wadhifa fulani na rais baada ya siku chache, tunaona au kusikia kuwa ameapishwa, lakini kwa Dk Slaa ni zaidi ya mwezi sasa, kuna sababu zimetolewa? Tujulisheni,” ni moja kati ya simu nyingi za wasomaji wetu waliopiga chumba cha habari kutaka ufafanuzi.

Kutokana na hali hiyo, Uwazi liliwasiliana na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu ili kujua kwa nini imechukua muda mrefu kumuapisha Dk. Slaa.
Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa, aliliambia gazeti kwa njia ya simu kuwa, si Dk. Slaa peke yake ambaye hajaapishwa.

“Utaratibu ukikamilika ataapishwa. Na sio yeye peke yake ambaye hajaapishwa,” alisema kwa kifupi Msigwa bila kuingia kwa undani zaidi kuhusu suala hilo.
Siku chache baada ya kutangazwa kushika nafasi hiyo, Dk. Slaa alikaririwa akisema anashukuru Mungu kwa kuteuliwa na rais.

Dk. Slaa kwa sasa yupo Canada na alitimkia nchini humo baada ya kutangaza kujiuzulu nafasi ya ukatibu mkuu Chadema.
Aliondoka Chadema baada ya kuwepo sintofahamu kati ya viongozi wa chama hicho, baada ya kumpokea waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa aliyehama CCM.
Lowassa ndiye alipewa baraka za kupeperusha bendera ya urais kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) iliyoshirikisha vyama vya Chadema, CUF, NCCR na NLD katika Uchaguzi Mkuu wa 2015.

Pamoja na kupewa ridhaa hiyo, alishindwa kufurukuta na hatimaye Dk. Magufuli kuibuka kidedea kwa nafasi ya urais kupitia CCM.
Itakumbukwa kuwa jina la Dk. Slaa lilianza kufahamika nchini kwa kasi kubwa wakati akiwa mbunge wa Jimbo la Karatu kupitia Chadema.

Kufahamika huko kulitokana na kusimama kidete kupiga vita rushwa kiasi kwamba alitetemesha baadhi ya viongozi waliokuwa madarakani kwani aliwataja.

Uhodari wake katika vita hiyo unaelezwa kuwa ndiyo uliomfanya Rais Magufuli kuguswa naye kiutendaji na kumteua kushika nafasi hiyo.
Dk. Slaa ana historia ndefu ya uongozi kwani aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) alipokuwa padre kabla ya kuingia kwenye siasa.

Baraza hilo ni chombo cha juu katika masuala mbalimbali ya usimamizi wa mambo ya Kanisa Katoliki nchini.
Katika andiko la Profesa Kitila Mkumbo ambaye kwa sasa ni Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji ni kwamba, Dk. Slaa alijitoa rasmi kwenye upadri mwaka 1991.
Kwa mujibu wa andiko hilo, Dk. Slaa aliacha nafasi hiyo kwa kufuata taratibu kamili za Kanisa Katoliki na aliacha mwenyewe bila kushinikizwa, kufukuzwa au kupewa onyo. 
Read more »

Siri ya Ndoa ya Dogo Janja na Uwoya Yafichuka Ukweli Huu Hapa

Siri ya Ndoa ya Dogo Janja na Uwoya Yafichuka Ukweli Huu Hapa

Siri ya Ndoa ya Dogo Janja na Uwoya Yafichuka Ukweli Huu Hapa

 10:00  
Msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye pia ni kama baba mlezi wa msanii Dogo Janja, Madee Senesa, ametoa sababu iliyowafanya wafanye siri kufungwa kwa ndoa ya Dogo Janja na Uwoya.


Akizungumza kwenye eNewz ya East Africa Television, Madee amesema walijua kuwa wawili hao ni maarufu, hivyo taarifa za ndoa yao ingewashangaza wengi na kuharibu mipango yote.

“Nilijua ni habari kubwa, ni habari ambayo ingeleta purukushani kwa wanahabari hata ndoa yenyewe isingefanyika, na hata wale ambao tumewaalika tulijua hawa wana marafiki zao ambao ni wana habari, hivyo tulichokifanya ni kutengeneza usiri wa ile shughuli, hata tuliowaalika tuliwaambia mnakuja hapa lakini simu zenu wekeni hapa, unangia unashuhudia tukio lakini hauna ushahidi wa kupeleka kwa wengine”, amesema Madee.

Madee ameendelea kwa kusema kwamba iwapo wasingefanya siri huenda wangetokea watu wa kuwashauri vinginevyo, na ndoa hiyo isingefungwa.

“Tungesema tuanze kuwaalika wangeanza kuwashauri usikubali kuolewa na yule au kumuoa huyu, ile ndoa ingekufa na sisi tungepata dhambi”, amesema Madee.

Mwezi Novemba mwaka 2017 msanii Dogo Janja na Irene Uwoya walifunga ndoa, jambo ambalo  liliwashtua watu wengi, huku wengine wakisema ni kiki ya filamu. 
Read more »

Maneno ya Ridhiwan Kikwete baada kuiona video ya Fresh Remix, adai Fid Q katii kauli ya Rais


December 12, 2017 President  Magufuli aliwataka Jumuiya ya Wazazi ya CCM kutokaa kimya  wanapoona mambo mabaya katika jamii na akasema kuwa amekuwa akikerwa na tabia ya baadhi ya wanawake kwenye video za wasanii wa bongo kuvaa vibaya na kuonyesha maumbile yao. ya ndani.
Leo January 4, 2018 Mbunge wa Chalinze (CCM) Ridhiwani Kikwete amempongeza Fid Q baada ya kuonesha kutii kauli ya JPM ambayo aliitoa kwenye Kamati Kuu ya CCM.
Ridhiwani ametoa pongezi hizo kupitia account yake ya Twitter baada ya kuiona video mpya ya Fid Q  aliyomshirikisha Diamond Platnumz na Rayvanny  ‘Fresh Remix’ ambapo ndani Video Queens wameonekana kuvaa magauni marefu ambayo yamewasitiri.
“Hii inaitwa tii bila shuruti. Hongera sana mdogo wangu Diamond, Fid Q kwa kuonyesha usikivu. Mavazi mazuri ni yale yanayohifadhi utu na jinsi. Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo” – Ridhiwani Kikwete

Hii inaitwa Tii Bila Shuruti. Hongera sana Mdogo wangu @diamondplatnumz , @FidQ kwa kuonyesha usikivu. Mavazi Mazuri ni Yale yanayohifadhi Utu na Jinsi. 
Read more »

VIDEO: MSANII UGANDA AMPIGIA MAGOTI SAIDA KAROLI KAFUNGUKA SABABU


Msaanii wa nyimbo za asili nchini Saida Karoli alikuwa ndo msanii pekee kutokea Tanzania aliyepata mualiko katika sherehe ya kufunga Mwaka nchini Uganda ambapo alitoa burudani na wasanii wa nchini humo na miongoni mwa wasanii waliokuwepo kwenye show hiyo ni pamoja na Hanson Baliruno.
Hanson Baliruno ni msanii kutoka Uganda ambaye alimpigia magoti Saida Karoli wakati wa show na kuelezea jinsi anavyo mkubali mkongwe huyo wa nyimbo za asili, Bonyeza PLAY hapa chini kumsikiliza Baliruno akielezea kwanini alimpigia magoti Saida…

Shangwe alilolipata SAIDA KAROLI kwenye kufunga mwaka UGANDA
Balaa la Queen Darleen Maisha Club, Lavalava amepanda peku kwenye stage
Read more »

Monday 1 January 2018

Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein: Kinga ni bora kuliko tiba

 Dk. Shein aliyasema hayo leo katika hotuba yake aliyoitoa  katika maadhimisho ya siku ya mazoezi Kitaifa yaliyovishirikisha vikundi mbali mbali vya mazoezi kutoka Unguja, Pemba na Tanzania Bara pamoja na vikosi vya SMZ yaliyoanzia katika uwanja wa Tumbaku na kuishia katika uwanja wa Amaan mjini Zanzibar yaliosimamiwa na Chama Cha Mazoezi ya Viungo Zanzibar (ZABESA).
Viongozi mbali  mbali walishiriki katika maadhimisho hayo akiwemo Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd pamoja na viongozi wengine wa Seriali na vyama vya siasa na wananchi ambapo katika maelezo yake Dk. Shein alisisitiza kuwa kufanya mazoezi kunasaidia kupunguza uzito wa mwili na kuwataka wananchi kufanya mazoezi na kutosubiri hadi wakaambiwa na daktari.
Dk. Shein aliwasisitiza wananchi kuzingatia usemi maarufu wa mabingwa wa lugha ya kiswahili kwamba “Tahadhari kabla ya athari” na “Kinga ni bora kuliko tiba”, hivyo alisisitiza ni vyema kila mmoja akajiwekea muda maalum wa kufanya mazoezi yanayolingana na afya na umri wake.
Pia, Dk. Shein alitangaza rasmin kuwa maadhimisho hayo ya Siku ya Mazoezi Kitaifa hapo mwakani yatafanyika Kisiwani Pemba huku akiitaka Wizara ya Habari,  Utalii, Utamaduni na Michezo kukitafutia ofisi Chama Cha Mazoezi ya Viungo Zanzibar (ZABESA) ili kiweze kufanya kazi zake kwa ufanisi zaidi.
Read more »

Hamisa Mobetto anyanyua mikono juu kwa Zari

Hivi karibuni kumekuwa na maneno mengi sana kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana ishu nzima ya Zari na hamisa kurushiana vijembe kwenye mitandao ya kijamii kisa kikidaiwa ni Diamond.
Ambapo kila mtu ameonyesha kusema ya kwake kwa upande wake na kutafsiriwa tofauti na vitu kama hivyo…..,na mwisho wa siku watu wakatafsiri kuwa Diamond yupo upande wa Zari though alimkosea na Zari kuonekana kumsamehe Diamond na kuwa pamoja hadi sasa, hivyo muendelezo wa vijembe vya Zari na Hamisa vilikuwa vinatafsirika kama kumgombea Diamond.
Kupitia snapchat account ya Hamisa amepost maneno yanayosema nani yupo tayari kuingia mwaka 2018 akiwa single yaani bila mwanaume, post hiyo imetafsirika kama Hamisa amekubali kuendelea na maisha mapya 2018 bila kuwa na mahusiano na diamond ni kama amekubali yaishe tu
Kwani Diamond ameamua kuwa na Zari jumla, kama ufahamu tu Hamisa na Diamond wamezaa mtoto mmoja wa kiume kwa upande wa Hamisa anamuita Abdulatif na Diamond anamuita Dylan.
Read more »

Video mpya ya Rayvanny ft Nikki wa Pili ‘Siri’



Video mpya ya Rayvanny ft Nikki wa Pili ‘Siri’


Msanii wa muziki Bongo, Rayvanny ameachia video ya ngoma yake mpya ‘Siri’ akiwa amemshirikisha Nikki wa Pili, video imeongozwa na Eris Mzava ambapo ndani ya video hiyo anaonekana  Baby Mama wake, Fahyma.
Itazame hapa.
Read more »

Picha: Mhe. Samia akijumuika na Wazee wa CCM kuukaribisha mwaka mpya 2018

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amejumuika na Wazee wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) katika kuukaribisha mwaka mpya wa 2018 kwenye makazi yake yaliyopo Tunguu, Wilaya ya Kati, mkoa wa Kusini Unguja Zanzibar.

Read more »

THIS BLOG DESIGNED BY

HOME BOYZ GRAPHICS LABORATORY